Maswali ya ndoa yanapelekwa huku

Swali: Nilimkataza mke wangu vazi ambalo wanachuoni walitoa Fatwa kutojuzu kulivaa kwa kumwambia “wewe kwangu ni haramu [ukivaa]”. Mara ya kwanza akaitikia, lakini hata hivyo akalivaa kwa mara ya pili kwa kusahau – kama alivyosema. Ni lipi la wajibu juu yangu katika hali kama hii?

Jibu: Masuala haya yanahitajia kuzingatiwa. Ni jambo lenye julikana ya kwamba watu ni wenye kupewa udhuru [wakati wa kusahau]. Allaah Amesema:

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا

”Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake.” (02:286)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ummah wangu ni wenye kusamehewa makosa ya kusahau na waliyotenzwa nguvu.”

Masuala haya yanatakiwa kuzingatiwa. Ninachomnasihi muulizaji aende [katika baraza] la kufutu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=11647
  • Imechapishwa: 01/05/2015