Swali: Tunasikia baadhi ya watu wanasema ´Qadar imetaka`. Je, msemo huu una makosa katika upande wa ´Aqiydah?

Jibu: Ndio. Haitakikani kusema hivi. Badala yake anatakiwa aseme ´Allaah Akitaka`. Asiyanasibishe matakwa kwa Qadar. Matakwa ni ya Allaah. Inatakikana kuacha msemo huu. Matakwa ni Sifa miongoni mwa Sifa za Allaah. Badala yake aseme ´Allaah Akitaka`. Ama kuhusu Qadar ni yale Aliyopanga na Kukadiria Allaah. Ni matendo ya Allaah. Hivyo asiseme ´Qadar ikitaka`. Badala yake aseme ´Allaah Akitaka´.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=11647
  • Imechapishwa: 01/05/2015