Anayemuuguza mgonjwa na swalah ya mkusanyiko

Swali: Je, inafaa kwa mwanamme mmoja au wawili kukaa pamoja na mgonjwa mwenye maradhi makali kama alivofanya al-´Abbaas na ´Aliy bin Abiy Twaalib?

Jibu: Ndio. Mgonjwa ni mwenye kupewa udhuru. Vivyo hivyo yule mwenye kuchelea juu ya nafsi au mali yake ni mwenye kupewa udhuru kuacha swalah ya mkusanyiko. Ikiwa yule ambaye anachunga mali swalah ya mkusanyiko inadondoka kwake, basi yule ambaye anachelea juu ya mgonjwa ana haki zaidi ikiwa anamuhitajia. Ama ikiwa hachelei juu yake na wala hakuna khatari juu yake, basi aende kuswali pamoja na mkusanyiko. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye mbora wa watu. Hapana shaka kwamba watu walikuwa wakipata uzito juu ya maradhi yao na walikuwa wakichelea juu yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (19)
  • Imechapishwa: 24/03/2021