Anataka kwenda msikitini lakini anaweza tu kuswali kwa kulala

Swali: Mtu anaweza kuja msikitini, hata hivyo anaweza tu kuswali kwa kulala na si kwa kuketi chini. Atasimama vipi katika safu?

Jibu: Aswali nyumbani kwake.

Swali: Anaweza kuswali kwa kulala msikitini, lakini hawezi kuswali kwa kuketi chini.

Ibn Baaz: Hawezi kuswali kwa kuketi mkao mwingine mbali na mutarabbiy´[1]?

Muulizaji: Nalala chali. Ni lazima niketi mkao huu.

Jibu.: Asije. Aswali nyumbani kwake. Ni mwenye kupewa udhuru.

[1] Ni mkao wa heshima ambao unakalia makalio kisha wakunja miguu kwa kuingiza mguu wa kulia ndani ya mguu wa kushoto.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23286/حكم-من-لا-يستطيع-الصلاة-الا-مستلقيا
  • Imechapishwa: 21/12/2023