Anataka kuondosha mti unaoendewa na makhurafi

Swali: Katika mji wangu kuna mti ambao watu wanasafiri kuuendea na wanatundika hirizi juu yake na ukurubisho. Mfano wa mambo haya yanapatikana kwa wingi. Je, inajuzu kwangu kuukata pamoja na kujua ya kwamba nikiukata huenda nikadhuriwa na kufungwa? Je, nikiuacha kunaingia katika kunyamazia maovu?

Jibu: Kusema uuondoshe mti huo huwezi isipokuwa mpaka uwe uko na sapoti ya serikali. Ikiwa una sapoti hiyo unaweza kuuondosha kwa mkono wako. Ikiwa huna sapoti ya serikali, unachotakiwa ni kulingania katika Tawhiyd na kukataza shirki na kubainisha kuwa mti huo haudhuru na wala haunufaishi. Wakikukubalia himdi zote ni za Allaah na wasipokukubalia utakuwa umetekeleza lililo la wajibu juu yako. Lililo la wajibu kwako ni kulingania katika dini ya Allaah. Kuhusiana na kuuondosha hili linahitajia serikali.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (08) http://alfawzan.af.org.sa/node/2123
  • Imechapishwa: 05/07/2020