Kuwakhabarisha watu maamrisho na makatazo ya ndoto  

Swali: Kuna wanaosema kuwa wamemuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na baada ya hapo anaenda kuwakhabarisha watu kuwa amemuona na kwamba amesema kadhaa na kadhaa. Je, wasadikishwe katika haya?

Jibu: Kuhusiana na kuwakhabrisha maamrisho na makatazo haijuzu. Baada ya kufa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuna maamrisho na makatazo. Maamrisho na makatazo yamo katika Qur-aan na Sunnah peke yake. Ama ndoto hakuthibiti kwayo amrisho wala katazo kwa hali yoyote. Asiwakhabarishe watu hili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (08) http://alfawzan.af.org.sa/node/2123
  • Imechapishwa: 05/07/2020