Anawaomba Malaika wamuamshe kuswali

Swali: Je, inajuzu kuwanadi Malaika walioko pamoja kutaka msaada kutoka kwao wa kuamshe kuswali usiku?

Jibu: Umejuaje kuwa wako pamoja na wewe? Je, unawaona? Haijuzu kufanya hivi. Ndugu yako anaweza kukusaida kukuamsha kuswali usiku au unaweza vilevile kuweka alamu ya kukuamsha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (08) http://alfawzan.af.org.sa/node/2123
  • Imechapishwa: 05/07/2020