Swali: Kuna ambao wanasema sababu ya uharamu wa picha ni kuabudu picha hizo na masanamu. Lakini kwa leo sababu hiyo imeondoka na kwa ajili hiyo picha inajuzu. Vipi mtu atajibu hilo?

Jibu: Ni kitu gani kimeondosha sababu hii? Sababu itaendelea kuwepo mpaka siku ya Qiyaamah. Jinsi wakati unavyozidi kwenda na ujinga kuenea ndivyo jinsi fitina inazidi kuwa nyingi juu ya hili. Vipi mtu huyu atasema hivi ilihali anawaona waabudu makaburi, waliofungamana na mambo ya athari na kutabarruk kwa athari hizo? Vipi atathubutu kusema hivi? Si kweli. Bali leo majanga yamezidi kuwa mengi kwa sababu ya ujinga, wakati umeenda zaidi na fitina zimezidi kuwa nyingi. Kisha jinsi wakati utakavyozidi kusonga mbele ndivyo jinsi ugeni utazidi kuwa mwingi na fitina. Haya ni maneno batili. Kusema kuwa imeisha ni maneno batili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (08) http://alfawzan.af.org.sa/node/2123
  • Imechapishwa: 04/07/2020