Anataka kujazia mke wa nne kabla ya kumalizika kwa eda ya aliyemwacha

Swali: Ni ipi hukumu ya Shari´ah tukufu juu ya mwanamme ambaye ameoa wanawake wane ambapo akamtaliki mmoja wao talaka ya kwanza. Katikati ya eda ya yule mwanamke akataka kumuoa mwanamke mwingine ili kukamilisha idadi ya wake wanne. Je, Shari´ah inamruhusu kuoa kabla ya kumalizika kwa eda ya yule mtalikiwa?

Jibu: Haijuzu kwake kuoa mwanamke wa nne kabla ya kumalizika kwa eda ya yule mwanamke wa nne ambaye kamtaliki ikiwa talaka ni ya kuweza kurejea. Haya ni kwa maafikiano ya waislamu wote. Kwani mtalikiwa awezaye kurejea ana hukumu kama ya wake wengine. Lakini ikiwa ni talaka ya tatu, kuoa mwanamke wa tano ni jambo wanachuoni wametofautiana. Salama zaidi ni yeye kuacha kufanya hivo mpaka imalizike eda ya yule mtalikiwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (22/177)
  • Imechapishwa: 28/12/2020