Mafunzo ya Uislamu juu ya kuwatenganisha watoto katika malazi

Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“… na watenganishe baina yao katika malazi.”

amekusudia kutenganisha kati ya watoto wa kiume na watoto wa kike wakati wa kulala kwa sababu wamekurubia wakati wa kubaleghe. Shaytwaan anaweza kuwapambia machafu kama vile kuingiliana nyuma na kadhalika.

Watoto wanapofikisha miaka kumi wanatakiwa kutenganishwa kwenye malazi. Ni lazima kati yao kuweko kizuizi. Lakini haina neno kama ni mtoto wa miaka minne, mitano au misita. Kwa sababu watoto wa miaka hiyo hawana hisia na hawezi kufanya kitu.

Katika mafunzi haya ya dini kuna kheri, uongofu na wema. Hakuna kheri yoyote isipokuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewaelekeza Ummah wake kwayo na wala hakuna shari isipokuwa amewatahadharisha nayo. Endapo watu wangetendea kazi mafunzo haya matukufu basi mambo yao yangelitengemaa katika mambo ya dunia na ya Aakhirah yao.

Uzindushi!

Tazama namna ambavo chaneli za satelaiti zinavyorusha shari na majanga kwa watu. Zinawafunza uhalifu, uzandiki na mambo ya ngono. Wamepatikana baadhi ya wale ambao wanatazama chaneli hizi wenye kuwafanyia machafu dada zao na wamekiri kwamba ni kwa sababu wameyaona hayo katika chaneli hizo na ndio maana na yeye akataka kumwigiliza. Amemfanyia uchafu dada yake. Haya ni majanga, shai na fitina zilizofunguliwa kwa waislamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kuwatenganisha watoto katika malazi na chaneli hizi za satelaiti zinafunza watu uhalifu, mambo ya ngono na zinawazoweza machafu. Chaneli hizo zinawasahilishia jambo la uzinzi na kuingiliana nyuma. Tunamuomba Allaah usalama na afya.

Kwa hivyo ni lazima kwa muislamu kuisafisha nyumba yake kutokamana na chaneli hizi chafu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 16-17
  • Imechapishwa: 28/12/2020