Swali: Mama yangu alifariki kitambo kidogo. Je, inafaa kwangu kufunga kwa ajili yake? Ikiwa siwezi kumfungia, kipi naweza kufanya kwa ajili yake?

Jibu: Hakufungwi wala kuswaliwa kwa ajili ya maiti. Isipokuwa kama alikufa na huku anadaiwa swawm ya wajibu. Mfano wa funga za lazima ni kama swawm ya kafara au swawm ya Ramadhaan na hakuwahi kulipa. Katika hali hiyo inapendeza kwa jamaa zake kumlipia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anayekufa na anadaiwa swawm, basi atafungiwa na walii wake.”

Bi maana ndugu zake.

Anapofariki na anadaiwa swawm ya Ramadhaan au swawm ya kafara, basi inapendeza kwa ndugu zake kumfungia. Kuhusu swawm inayopendeza asifungiwe na wala asiswaliwe. Hata hivyo atolewe swadaqah ya pesa, aombewe du´aa ya msamaha, rehema na kadhalika.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/17027/حكم-الصوم-عمن-ليس-عليه-صوم
  • Imechapishwa: 22/03/2023