Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke kusafiri kwa ajili ya kulingania?

Jibu: Anamwabudu Allaah kwa maasi? Haijuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Si halali kwa mwanamke anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho kusafiri umbali wa siku mbili isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”

Maana ya ´si halali` ni kwamba ni haramu na maasi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14041434.mp3
  • Imechapishwa: 14/04/2023