Kununua nyumba au hajj kwanza?

Swali: Kuna mtu anataka kuhiji na yuko na pesa ya kununua nyumba. Je, atangulize hajj au kununua nyumba?

Jibu: Atangulize mahitaji yake ya msingi. Nyumba ni katika mahitaji yake ya kimsingi. Anahitaji nyumba. Kwa hivyo anunue nyumba. Baada ya hapo kile chenye kuzidi mahitaji yake ndio ahiji nacho.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14041434.mp3
  • Imechapishwa: 14/04/2023