Swali: Ni zipi nasaha zako juu ya mtu ambaye anamtukana na kumtahadharisha Shaykh al-Albaaniy? Tunatakiwa tuchukue msimamo gani juu ya bwana huyu?

Jibu: Haya ni miongoni mwa maajabu makubwa kuona Shaykh al-Albaaniy anatahadharishwa, mtu ameitumikia Sunnah na kumaliza uhai wake katika kuzisoma Hadiyth za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kuzihakiki na kubainisha ambazo ni Swahiyh na ambazo si Swahiyh. Kinyume chake inatakikana kwa mtu amwombee du´aa, amsifu na afaidike kutokana na elimu yake. Hii leo mtu ambaye anajishughulisha na Hadiyth hawezi kujitosheleza kurejea kwa watu wawili: Haafidhw Ibn Hajar na Shaykh al-Albaaniy. Faida inayoweza kuchumwa katika mambo yanayohusiana na Hadiyth kutoka kwa Ibn Hajar na Shaykh al-Albaaniy ni kubwa. Kwa ajili hiyo yule ambaye anamtahadharisha Shaykh al-Albaaniy basi anatahadharisha juu ya maarifa ya haki na Sunnah. Yale aliyofanya Shaykh al-Albaaniy juu ya Hadiyth ni huduma ya kipekee na uangalizi mtimilifu juu ya Sunnah na namna inavyotakiwa kutendewa kazi na kupokelewa na wanafunzi. Anastahiki kusifiwa na kuombewa du´aa.

  • Mhusika: ´Allâmah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbâd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=8mg9016GYTk
  • Imechapishwa: 30/08/2020