Josho linaondosha hadathi ndogo na kubwa?

Swali: Je, josho linaondosha hadathi ndogo pindipo mwanamme au mwanamke atanuia jambo hilo na hivyo itamtosheleza kutokamana na kutawadha?

Jibu: Wako wanachuoni wenye kuona hivo. Wanachuoni wametofautiana juu ya mambo haya. Baadhi ya wanachuoni wanaona kuwa mtu akioga na wakati huohuo akanuia kuondosha hadathi ndogo na hadathi kubwa basi inaondoka. Isipokuwa ikiwa kama atapata hadathi katikati ya josho kama vile kutokwa na upepo au akagusa tupu yake. Katika hali hiyo atatakiwa kutawadha. Lakini akioga na wakati huohuo akanuia kuondosha hadathi zote mbili basi baadhi ya wanachuoni wanaona kuwa inaondoka. Wanachuoni wengine wameona kuwa ni lazima atawadhe mwanzo, kama alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kisha ndio atakamilishe josho lake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (15)
  • Imechapishwa: 30/08/2020