Swali: Je, inafaa kwa mwanamke wa Kiislamu kutoka kwa wingi nje ya nyumba kwa ajili ya kulingania kwa Allaah?

Jibu: Hiki ni kitendo chema. Mwanamke kutoka kwa ajili ya kulingania ni kitendo chema. Maneno Yake:

وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ

“Kaeni majumbani mwenu.”[1]

Maamrisho ya kutulizana nyumbani ni pale ambapo hakuna haja. Lakini kukiwa kuna haja, kwa mfano kutoka kwa ajili ya kutoa mawaidha, ukumbusho kati ya wanawake, kutoka kwa ajili ya kuswali mkusanyiko pamoja na wanamme kutokana na manufaa aliyoona na wakati huohuo akavaa Hijaab na kujisitiri, itambulike kuwa wanawake wa Maswahabah walitoka katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa ajili ya kuswali pamoja naye msikitini mwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pamoja na kuvaa Hijaab na kujisitiri. Vivyo hivyo mwanamke anaweza kutoka kwa ajili ya kuwatembelea wazazi wake wawili na jamaa zake wa karibu pamoja na kuvaa Hijaab na kujisitiri. Pia anaweza kutoka kwa ajili ya kwenda kumtembelea mgonjwa, kumpa pole mfiliwa, kulingania katika dini ya Allaah au mfano wa hayo katika makusudio mazuri. Lakini achunge yale ambayo Allaah ameamrisha katika Hijaab na sitara na asijishauwe kuonyesha mapambo yake na kutojitia vitu vya fitina.

Wanawake wanahitajia ulinganizi kama jinsi wanaume wanavohitajia. Kila mmoja anahitajia Da´wah. Ni sawa pia endapo mwanamke huyo atawanasihi na kuwawaidhi wanamme. Tumekwishatangulia kusema kwamba sauti ya mwanamke sio ´Awrah. Sauti yake wakati wa kulingania katika dini ya Allaah, kuelekeza katika kheri na kukemea maovu sio ´Awrah. ´Awrah kama tulivyotangulia ni pale ambapo atakiuka na kuleza sauti.

[1] 33:33

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaad-ud-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4243/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%AE%D8%B1%D9%88%D8%AC-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B1%D8%A7%D8%A9-%D9%84%D9%84%D8%AF%D8%B9%D9%88%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D9%89-%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87-%D8%AA%D8%B9%D8%A7%D9%84%D9%89
  • Imechapishwa: 30/08/2020