Swali: Ni yepi maoni yenye nguvu juu ya ambaye anaacha swalah hali ya uvivu na uzembe? Je, anakuru kwa kitendo hicho?

Jibu: Ndio, anakufuru. Udhahiri wa Hadiyth ni kwamba anakufuru. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Yule mwenye kusahau swalah au akapitikiwa na usingizi, basi aiswali pale atakapoikumbuka. Haina kafara nyingine isipokuwa hiyo.”[1]

Aliyeacha kwa makusudi anatakiwa kutubu kwa Allaah. Anatakiwa kuharakisha kutubia na kuanza kuswali.

[1] al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (39)
  • Imechapishwa: 03/06/2023