Anafunua uso wake mbele ya shemeji zake wanaokariba baleghe

Swali: Nina kaka ambaye umri wake ni miaka kumi na mbili na mke wangu anafunua uso wake mbele yake. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Anatakiwa kujisitiri mbele yake. Kwa sababu huyu amekaribia. Pengine akawa amekwishabaleghe na ni mwenye kuota. Huenda nywele zake za sehemu ya siri zimekwishaota ingawa ni mtoto wa miaka kumi na mbili. Anaweza kubaleghe katika miaka hii. Kwa ajili hiyo mwanamke anapaswa kujisitiri kwa ambaye amekaribia kubaleghe. Akiwa ni mtoto wa miaka kumi anayeelewa [mambo ya wakubwa] basi unapaswa kujisitiri mbele yake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (21)
  • Imechapishwa: 04/09/2021