Swali: Niliswali na rafiki yangu na mimi ndiye nilikuwa imamu. Rafiki huyu alikuwa mchezi mwenye furaha. Akaniinamia nikiwa ndani ya swalah na kicheko kikanishinda. Nikavumilia licha ya hivo nikatokwa na sauti inayofanana na kicheko. Kisha nikakamilisha swalah yangu. Ni kipi kinachonilazimu?

Jibu: Ikiwa kitendo chako ni cha kutabasamu basi tabasamu haiharibu swalah. Ama ikiwa ni kicheko kweli, basi kicheko hicho kinaharibu swalah. Ahnaaf wanaona kuwa kicheko cha kweli kinaharibu swalah na wudhuu´ vyote viwili. Wanaona kuwa yule mwenye kucheka kweli basi swalah na wudhuu´ wake vibaharibika. Maoni ya sawa ni kwamba wudhuu´ hauchenguki isipokuwa akipatwa na hadathi na akatokwa na upepo. Lakini kicheko cha kweli kinaharibu swalah. Ama ikiwa ni kutabasamu tu hakuharibu swalah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (21)
  • Imechapishwa: 04/09/2021