an-Naas na al-Falaq zinazotosha kutokana na kinga nyenginezo?

Swali: Je, imepokelewa kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati iliposhuka “an-Naas” na “al-Falaq” aliacha mengine yote aliyokuwa akiomba kinga kwayo?

Jibu: Siyakumbuki hayo. Lakini amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakujilinda mwenye kujilinda kwa mfano wa hizo mbili.”

Inapendeza kwa muumini kuzisoma baada ya kila swalah. Asome al-“Ikhlaasw”, “an-Naas” na “al-Falaq” baada ya kila swalah, wakati wa kulala mara tatu. Yote haya ni kwa lengo la kujilinda. Kama ambavo mtu anatakiwa kufanya sababu nyenginezo kukiwemo kufunga mlango wake, amtaje Allaah kabla ya kula na kunywa. Hizi ni sababu. Haifai kwake kuacha kula na kunywa mpaka akafa. Anatakiwa kufanya sababu nyenginezo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23104/هل-يكتفى-بالمعوذتين-عن-ساىر-التعوذات
  • Imechapishwa: 03/11/2023