Swali: Baadhi ya wanazuoni wamesema kuwa Adhkaar zilizopokelewa zinazomkinga mtu kutokana na nyoka, nge na mashaytwaan ni kama upanga mkononi mwa mpiganaji; akiwa ni mwenye nguvu utamsaidia, na akiwa ni mwenye imani dhaifu hautomsaidia.

Jibu: Makisio. Hili ni kwa njia ya makisio. Mtu anatakiwa kuzisoma na kumtarajia Mola wake. Kwa msemo mwingine asiwe mwenye kujiaminisha na wala asiwe mwenye ikhlaasw dhaifu na matarajio dhaifu. Bali azisome na atambue kuwa ni sababu. Sambamba na hilo awe mkweli, kumdhania Allaah vyema, kumtarajia na kumsadikisha Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23103/هل-يكون-اثر-التعوذات-بقدر-قوة-الداعي
  • Imechapishwa: 03/11/2023