Kutoka kwa Muhammad bin Ibraahiym kwenda kwa muheshimiwa ´Abdur-Rahmaan bin Muhammad bin ´Aliy.
السلام عليكم ورحمة الله وبركاته
Tumefikiwa na barua yako ambayo unauliza juu ya swawm ya mama yako na umetaja kwamba amefunga miaka tisa na maradhi yakamzidi mpaka amefikia hali ya kwamba anapoteza hisia na hawezi kuongea. Wakati mwingine akihisi nafuu anapata hisia na anaweza kuongea. Hata hivyo hakufunga Ramadhaan miaka yote hii na kwamba hatimaye akaaga dunia mwishoni mwa Sha´baan mwaka huu. Je, anapaswa kulipiwa au kutolewa chakula?
Kuhusu ule muda ambao alikuwa amepoteza fahamu swawm ni yenye kudondoka kutoka kwake. Kuhusu kile kipindi ambacho alipata nafuu, ikiwa aliweza kufunga, basi anatakiwa kutolewa chakula kwa niaba yake Mudd au nusu pishi kwa kila siku moja iliyompita kumpa masikini. Na ikiwa hakuweza kufunga mpaka akaaga dunia basi hakuna kinachomlazimu; si kumtolea chakula wala kitu kingine. Allaah ndiye mjuzi zaidi.
Muftiy wa Saudi Arabia
19/09/1385
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/185)
- Imechapishwa: 13/03/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Miaka sita ameshindwa kufunga na bado maradhi yanamwandama
Kutoka kwa Muhammad bin Ibraahiym kwenda kwa muheshimiwa X. السلام عليكم ورحمة الله وبركاته Tumefikiwa na barua yako unayouliza maswali mawili ambapo moja wapo ni kwamba unadaiwa swawm ya miaka sita kutokana na miezi sita na kwamba mwezi huu unaokuja utakuwa ni wa saba na kwamba huwezi kufunga na kwamba…
In "Mgonjwa katika Ramadhaan"
Amechelewesha kulipa siku zake za Ramadhaan kwa miaka tisa
Swali: Kuna mwanamke alipatwa na hedhi katika Ramadhaan na wala hakulipa siku zake isipokuwa baada ya miaka tisa kwa sababu ya ujinga wake. Je, kuna kinachomlazimu mbali na kulipa? Jibu: Akiwa ni mjinga hakuna kinachomlazimu. Kwa sababu ni mwenye kupewa udhuru. Jengine ni kwamba hakukusudia. Ikiwa atalipa pamoja vilevile na…
In "Swawm ya mwanamke"
Ni wajibu kwa mtu kulipa swalah na swawm ya yale masiku yaliyompita pindi alipokuwa amezimia?
Swali: Kuna mwanamke alipatwa na kiharusi kabla ya Ramadhaan na hakupoteza fahami kikamilifu. Alikuwa anapoanza kuswali katikati ya swalah anaanza kuwazungumzisha walioko pembezoni naye. Ilipokaribia Ramadhaan ndipo akapoteza fahamu kikamilifu. Lakini madaktari wakasema kuwa anasikia. Kisha baada ya hapo akafariki katika Ramadhaan. Je, atolewe kafara? Jibu: Mwanamke huyu ambaye alipatwa…
In "Mgonjwa katika Ramadhaan"