Amesitisha swawm ya kafara kutokana na maradhi

Swali: Niliangukia kwenye jimaa mchana wa Ramadhaan na sikuwa najua kuwa jimaa wakati mtu amefunga kunawajibisha kutoa kafara na kulipa. Baada ya kujua yanayonipasa katika kulipa na kutoa kafara nilinunua mfuko wa mchele na nikawagawia masikini na pia nikaanza kufunga. Nilikuwa nafunga mpaka nikakamilisha siku 57. Baada ya hapo niliugua maradhi makali ambayo sikuweza kufunga ambapo nikaacha kufunga kwa siku mbili. Kisha nikaendelea mpaka nikakamilisha siku 60. Je, hayo yanatosha kutokana na kafara?

Jibu: Umefanya vyema katika uliyoyafanya. Kukatisha kwa sababu ya maradhi haidhuru. Kwa sababu maradhi ni udhuru unaokubalika kwa mujibu wa Shari´ah. Kukata kwa sababu hiyo haidhuru. Zilipokamilika siku tatu baada ya hapo imesihi na kukamilika swawm yako na pia umetekeleza kafara. Ikiwa umefunga huna haja ya kuzidisha suala la kulisha chakula. Kulisha kunakuwa badala ya kufunga. Kufunga ndio jambo linalotangulia, lenye kusihi na ndio kafara inayolazimu baada ya kuacha mtumwa huru kwa ambaye ameshindwa kuacha mtumwa huru. Kuhusu kulisha chakula kunatakikana wakati mtu ameshindwa kufunga. Midhali umefunga hulazimiki kulisha chakula. Mkoba uliotoa utakuwa ni kitu cha ziada na jambo la kujitolea. Unapata thawabu kwayo mbele ya Allaah.

  • Mhusika: Imaam
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/13699/حكم-الافطار-في-كفارة-الجماع-لعذر-المرض
  • Imechapishwa: 26/03/2023