Ameshauriwa kutofunga daima kutokana na maradhi sugu lakini baadaye akapona

Swali: Kuna mtu alipatwa na maradhi sugu na madaktari wakamshauri asifunge daima. Lakini aliwaendea madaktari wa nchi nyingine na akapona kwa idhini ya Allaah na hayo yalitokea baada ya miaka tano. Zimempita Ramadhaan tano pasi na kufunga. Afanye nini baada ya Allaah kumponya? Je, azilipe au hapana?

Jibu: Ikiwa madaktari waliomshauri kutokufunga daima ni madaktari waislamu na waaminifu na wanaotambulika kuwa wataalamu wa maradhi haya na wakamwambia kuwa hatarajiwi kupona, basi halazimiki kulipa na inamtosha kulisha chakula [alikofanya]. Lakini analazimika kufunga katika mustakabali.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/12379/حكم-من-نصحه-الاطباء-بالافطار-لمرض-مزمن-ثم-برى
  • Imechapishwa: 26/03/2023