Amesahau kutaja jina la Allaah wakati wa kupiga

Swali: Muwindaji amesahau kutaja jina la Allaah wakati wa kupiga kwake risasi. Je, mnyama huyu ni halali?

Jibu: Si halali. Miongoni mwa sharti ni lazima ataje jina la Allaah wakati wa kumtuma. Akisahau, si halali. Wako wanazuoni wanaosema kuwa ni halali, kama ambavo mtu akisahau kutaja jina la Allaah wakati wa kuchinja ni halali. Lakini mawindo sio kama uchinjaji. Mawindo ni ruhusa na kwa ajili hiyo ni lazima kuchukua tahadhari kubwa zaidi kuliko kuchinjwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (42)
  • Imechapishwa: 08/12/2023