Amemwacha mke kwa familia yake na hataki kumtaliki

Swali: Mimi ni kijana nimeoa na mke wangu ni mjamzito. Nimemuacha kwa familia yake na sasa ana karibu mwaka. Mimi simpendi bali namchukia. Je, nina dhambi katika kumuacha?

Jibu: Ndiyo, ndiyo. Ikiwa anataka talaka basi unapata dhambi; ima umpe talaka au utekeleze haki yake. Ama ikiwa ameridhia na amekusamehe, anaomba usimwache na anatarajia Allaah kukuongoza na kwamba utarudi kwake, basi hakuna ubaya. Ama ikiwa anakataa na anakutaka utekeleze wajibu wake au umwache, basi ni juu yako utekeleze wajibu wako au talaka, mojawapo ya mambo mawili. Ama ikiwa yuko kwa familia yake na amesamehe na hataki talaka na wala hakuna mzozo, basi wewe fikiria na muombe Allaah mwongozo. Shauriana na marafiki zako na jamaa zako. Ikiwa yeye ni mwema, ni katika watu wa kheri, uongofu na amenyooka sawasawa, basi usimtaliki hata kama unamchukia. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

فَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَيَجْعَلَ اللَّـهُ فِيهِ خَيْرًا كَثِيرًا

“… pengine ikiwa mnachukia jambo na Allaah akalijaalia ndani yake kuwa na kheri nyingi.”[1]

Huenda ukirudi kwake nafsi yako ikatakata na ukaona kutoka kwake yanayokufurahisha na hivyo akakuvutia baada ya hapo. Kwa hiyo usifanye haraka.

[1] 04:19

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3464/حكم-ترك-الزوجة-عند-اهلها-وعدم-تطليقها
  • Imechapishwa: 02/09/2026