Hukumu ya kuoa msichana wa baba wa aliyenyonya pamoja nawe kutoka kwa mama yako

Swali: Ikiwa alinyonya pamoja na mimi kutoka kwa mama yangu mtoto wa kiume, na baba wa huyo mtoto akaoa mwanamke mwingine na akazaa naye msichana, je, inajuzu mimi kumuoa huyo msichana?

Jibu: Ikiwa alinyonya kutoka kwa mama yako mtoto wa kiume na ikawa kunyonyesha kamili mara tano, basi huyo mtoto anakuwa ndugu yako. Ama baba yake akioa mwanamke mwingine na akazaa naye msichana, basi huyo msichana si ndugu yako. Huyo ni msichana wa mke mwingine asiye mama yako. Huyo mtoto aliyenyonya anakuwa ndugu yako kwa sababu alinyonya kutoka kwa mama yako na alinyonya kutoka maziwa ya mume wa mama yako, naye ni baba yako. Ama baba wa huyo mtoto ambaye si wa kando, hana uhusiano na hili. Hakika huyu mtoto aliyenyonya kutoka kwa mama yako pamoja na wewe anakuwa ndugu yako, na watoto wake wa kike wewe unakuwa ami yao. Ama baba wa huyo mtoto, huna uhusiano na watoto wake. Wao ni wageni kwako. Hivyo inajuzu kwako kumuoa msichana wa huyo mtu ambaye ni ndugu wa yule aliyenyonya pamoja na wewe. Yeye ni ndugu yake, si ndugu yako. Lakini ni binti wa baba wa huyo aliyenyonya. Ama yeye (aliyenyonya) amekuwa ndugu yako kwa sababu alinyonya kutoka kwa mama yako, si kwa sababu ni mtoto wa fulani. Bali kwa sababu alinyonya kutoka kwa mama yako. Watoto wote wa mume ambaye ni mwenye maziwa, ikiwa yeye ni baba yako basi wao ni ndugu zako. Ikiwa ni mume wa mama yako, basi watoto wake aliowapata kutoka kwa mke mwingine wanakuwa ndugu zako kwa upande wa baba. Ama baba wa huyo mtoto aliyenyonya kutoka kwenu, yeye na watoto wake ni wageni kwako.

Swali: Hivyo inajuzu kumuoa?

Jibu: Ndiyo, ni mgeni.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3474/الاحكام-المترتبة-على-الرضاعة
  • Imechapishwa: 02/09/2026