Ameibiwa pesa aliokuwa amenuia kuitoa zakaah

Swali: Kuna mtu alikusanya pesa ili aitolee zakaah ardhi yake ilioko Misri. Akaibiwa pesa hiyo ya zakaah na matumizi yake binafsi huko Madiynah. Je, anazingatiwa kuwa amekwishatoa pesa ya zakaah kutokana na nia yake?

Jibu: Hapana, hajatoa zakaah mpaka awafikishe nayo kwa watu wake wenye kuiistahiki. Akiibiwa Allaah atampa nyingine bora zaidi. Hata hivyo analazimika kutoa zakaah. Analazimika kutoa zakaah hadi aifikishe kwa watu wake wenye kuiistahiki. Muda wa kuwa iko kwake anahesabika hajaitoa. Ni mamoja ameibiwa au ameitumia. Hajatoa zakaah mpaka aitoe.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22995/ما-حكم-من-اخرج-مال-الزكاة-فسرق-قبل-اداىه
  • Imechapishwa: 06/10/2023