Bora kuacha ziada katika Tasliym

Swali: Je, ziada inayosema ´na baraka Zake` (وبركاته) katika Tasliym imesihi?

Jibu: Imepokelewa katika Hadiyth hii. Haafidhw [Ibn Hajar] ametaja katika “Buluugh-ul-Maraam” ya kwamba ni sahihi. Lakini kikosi cha wanazuoni wengine wamesema kuwa kinapingana na zilizo Swahiyh. Kwa hivyo bora ni kusema tu:

السلام عليكم ورحمة الله

“Amani na baraka za Allaah ziwe juu yenu.”

Kama inavofanywa hii leo. Hivo ndivo ilivyothibiti katika “as-Swahiyh” ya Muslim kupitia kwa Samurah ambaye amesimulia kwamba:

“Walikuwa wanaposalimia ndani ya swalah husema:

السلام عليكم ورحمة الله

“Amani na baraka za Allaah ziwe juu yenu.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22983/هل-زيادة-وبركاته-في-التسليم-من-الصلاة-صحيحة
  • Imechapishwa: 06/10/2023