Ameamka baada ya jua kuchomoza

Swali: Kuna mtu ameamka kutoka usingizini baada ya jua kuchomoza na bado hajaswali Fajr. Je, inafaa kwake kuichelewesha Fajr mpaka wakati wa kupondoka kwa jua?

Jibu: Hapana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Yule mwenye kusahau swalah au akapitikiwa na usingizi, basi aiswali pale atakapoikumbuka. Haina kafara nyingine isipokuwa hiyo.”

Anapaswa kuharakisha kuiswali pasi na kujali ni wakati gani, hata kama ni katika wakati wa makatazo aiswali.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (39)
  • Imechapishwa: 01/06/2023