Imaam Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

“Sita: Mola Wake (Subhaanahu wa Ta´ala) alimzungumzisha, akamnong´oneza na akamwita. Ambaye kumejuzu kwake kuzungumza na kuongea na kumsikilizisha mzungumzishwaji maneno akaweza kuyasikia Maneno Yake wakiwa pamoja, bila ya kuwepo kizuizi chochote, basi kuonekana Kwake ni kitu cha aula zaidi juu ya kujuzu kwake.”

Wakati Allaah alipomzungumzisha Muusa ndipo akaamini kuwa Mola Wake anaonekana na akawa amemuomba kuweza kumuona. Maneno na Mzungumzaji kunafahamisha kuwa huyu mzungumzaji anaonekana. Lakini hata hivyo haujafika wakati wa kuonekana. Wakati wa kuonekana ni Aakhirah.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bayaan wa al-Idhwaah li ´Aqiydah Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy Ru´yati Allaahi yaum al-Qiyaamah, uk. 20
  • Imechapishwa: 27/08/2020