Imaam Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

Kuhusiana na maneno Yake:

لَن تَرَانِي

“(Lan) hutoniona!” (07:143)

Inafahamisha juu ya ukanushaji wa huko mbeleni na haifahamishi juu ya ukanushaji wa milele hata kama ukanushaji utaambatanishwa na umilele. Vipi iweje pale ambapo ukanushaji haukuambatanishwa na umilele! Amesema (Ta´ala):

وَلَن يَتَمَنَّوْهُ أَبَدًا

“Na (Lan) hawatoyatamani [hayo mauti] hata siku moja.” (02:95)

Pamoja na maneno Yake (Ta´ala):

وَنَادَوْا يَا مَالِكُ لِيَقْضِ عَلَيْنَا رَبُّكَ

“Wataita: “Ee Maalik [mlinzi wa Moto]! Na atumalize [tufe] Mola wako.” (43:77)

MAELEZO

Allaah amesema juu ya mayahudi:

وَلَن يَتَمَنَّوْهُ أَبَدًا

“Na (Lan) hawatoyatamani [hayo mauti] hata siku moja.”

Hapa Allaah anakusudia duniani. Hawatotamani mauti kamwe duniani. Amesema:

وَلَن يَتَمَنَّوْهُ أَبَدًا

“Na (Lan) hawatoyatamani [hayo mauti] hata siku moja.”

Kuhusiana na Aakhirah watapokuwa Motoni watayatamani na kuyapupia. Amesema (Ta´ala):

وَنَادَوْا يَا مَالِكُ لِيَقْضِ عَلَيْنَا رَبُّكَ

“Na wataita: “Ee Maalik [Mlinzi wa Moto]! Na atumalize [tufe] Mola wako.”

Bi maana atufishe. Watatamani mauti Aakhirah. Kwengine amesema:

وَلَن يَتَمَنَّوْهُ أَبَدًا

“Na (Lan) hawatoyatamani [hayo mauti] hata siku moja.”

Sio dalili yenye kuonesha kuwa Allaah hatoonekana Aakhirah. Ambapo haonekani ni duniani. Kuhusiana na Aakhirah ataonekana.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bayaan wa al-Idhwaah li ´Aqiydah Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy Ru´yati Allaahi yaum al-Qiyaamah, uk. 20
  • Imechapishwa: 27/08/2020