Ambaye ana haki zaidi ya kupewa zakaah na swadaqah

Swali: Kutokana na Aayah mtu anatakiwa kumpa zakaah ambaye ana hali mbaya zaidi kisha anayefuatia kwa hali m ya zaidi au inasihi kumpa mmoja wao?

Jibu: Kwa hali yoyote inasihi kumpa yeyote katika mafukara. Lakini vizuri na bora zaidi ni mtu kujitahidi kumtafuta yule mwenye kujizuilia zaidi kuwaomba watu na akajitahidi kumtafuta ambaye ana ufukara zaidi. Kwa hivyo yule mtoa zakaah anatakiwa kujitahidi kumtafuta ambaye ni muhitaji zaidi na ajitahidi kumtafuta ambaye ni mwenye kujizuilia zaidi kuwaomba watu. Hapana shaka kwamba kufanya hivo ndio bora.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21625/مسالة-في-الصدقة-على-الفقراء
  • Imechapishwa: 03/09/2022