Swali: Kuwasalimia maiti inakuwa pale mtu anapoingia makaburini au hata akipita pambizoni mwayo?

Jibu: Hadiyth inasema pindi mtu atapofika makaburini. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yatembeeni makaburi… “

Anayepita kwa kwa nje huenda asiwe na hukumu ya aliyeingia. Lakini akiwatolea salamu wakati amepita karibu nayo ni vizuri. Lakini pengine tusimpe hukumu ya ambaye ameingia ndani. Kwa sababu ambaye ameingia amekusudia kuyatembelea. Amepita tu na hakukusudia matembezi. Lakini akiwaombea msamaha amefanya vyema.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/هل-السلام-على-الأموات-يقال-عند-دخول-المقبرة-فقط-أو-حتى-عند-المرور-بجانبها
  • Imechapishwa: 12/06/2022