Kinachosemwa na maamuma wakati imamu anapomsifu Allaah

Swali: Waswaliji waseme kitu gani wakati imamu anapomaliza kusoma du´aa ya Qunuut kwa kumswalia na kumtakia amani Mtume Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam na kizazi chake? Vivyo hivyo wakati imamu anaposema:

ولا يعزّ من عاديت

“… na wala hapati nguvu yule Uliyemfanya adui.”

Wako wanaosema:

“Nashuhudia.”

Jibu: Aseme:

“Aamiyn.”

Kusema kwake:

ولا يعزّ من عاديت

“… na wala hapati nguvu yule Uliyemfanya adui.”

ni sentesi ya sababu. Lakini imefungamana na yaliyoko kabla yake. Kwa hiyo hakuna neno akasema “Aamiyn” pamoja nayo. Ama kusema:

“Nashuhudia.”

ni kitu ambacho hakikupokelewa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sa-altu Abiy, uk. 148-149
  • Imechapishwa: 03/07/2022