Swali: Mimi nimeoa takriban miaka miwili iliopita. Mimi na mke wangu daima tuna ugomvi. Sote tuna makosa kwa haki ya mmoja kwa mwenziwe. Tukapatakana kabla ya mwezi na nusu ya kwamba, kila mmoja amtimizie mwenziwe haki yake na aombe ile ambayo itakuwa ya kwake. Lakini kabla ya siku mbili alikosea mke wangu na akanipiga kipigo kikali. Na nilikaribia kutamka neno “Talaka” lakini nikaimiliki nafsi yangu na kumwambia: “Wewe ni haramu kwangu, wewe ni haramu kwangu kama mamangu.” Na sikuwa najua ya kuwa hii ni Dhwihaar na ni haramu. Na sikuwa nakusudia kumtalaka. isipokuwa ilikuwa ni kumuadhibu tu. Unatunasihi nini Shaykh wetu (Allaah akuhifadhi)? Na ni lipi la wajibu juu yangu na juu ya mke wangu?

Jibu: Ewe mwanangu! Kwa vile anakupiga, mimi naona kama hakufai. Nasaha yangu muache kwa wema. Hakika mimi najua wanawake wasiokuwa na elimu waume zao wanawapiga kipigo cha kipindukia na wala mwanamke hawezi kumnyooshea mkono. Haya ndio maumbile ya mwanamke mwenye akili, mwerevu na anamuheshimu. Ama unakasirika tu ndio unampiga?! Mimi nasema: “Allaah amkate mkono wake”. Ningelikuwa mahala pako nisingelimbakisha dakika hata moja, ningelimuacha kwa salama.

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.miraath.net/fatwah/6776
  • Imechapishwa: 22/09/2020