Mke anadai ana maradhi baada ya mume wake kuoa mke wa pili

Swali: Kuna dada kutoka Uingereza anauliza. Mume wangu ataoa mke wa pili, kisha [huyo mwanamke] akagundua ya kuwa ni mgonjwa kwa maradhi ambayo yanaambukiza kupitia jimai. Je, yule mke wa kwanza anaweza kumkatalia kulala nae mpaka mke aende kwanza kwa daktari kwenye uchunguzi ili asimuambukize ugonjwa huu?

Jibu: Jambo la kwanza, hivi kweli una uhakika? Au imekufikia tu ukawa ni mwenye kudhani tu?

Mche Mola Wako (Subhaanahu wa Ta´ala) ewe binti. Ukihakikisha hilo na ukawa na yakini, unaweza kumkatalia.

“Hakika utiifu ni katika wema.”

Na haya maradhi ambayo yanaambukiza kupitia jimai, ni lazima aambukizwe na kitu isipokuwa Akipenda Allaah. Mnasihi na amueleweshe ya kwamba hukumkatalia kwa ajili ya kumchukia wala kwa ajili ya kumfanyia uadui, lakini ni kwa ajili ya haya maradhi.

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.miraath.net/fatwah/6475
  • Imechapishwa: 22/09/2020