Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

وعن أبي حمزة أنس بن مالك الأنصاري- خادم رسول الله صلي الله عليه وسلم _ رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلي الله عليه وسلم: ((لله أفرح بتوبة عبده من أحدكم: سقط على بعيره، وقد أضله في أرض فلاة)) (متفق عليه)

15 – Hamzah Anas bin Maalik al-Answaariy (Radhiya Allaahu ´anh) – mtumishi wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah ni mwenye furaha mno kwa tawbah ya mja Wake kuliko mmoja wenu aliyeanguka kutoka juu ya ngamia wake na akampotea pindi alipokuwa katika ardhi ya jangwa.”[1]

Katika Hadiyth hii kuna dalili ya kufurahi kwa Allaah (´Azza wa Jall) juu ya tawbah ya mja Wake wakati anapotubia Kwake na kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anapenda hilo mno. Lakini hata hivyo sio kwa ajili ana haja ya matendo na tawbah zetu. Allaah ni mwenye kujitosheleza na sisi. Hilo ni kwa sababu Yeye (Subhaanah) anapenda ukarimu. Hakika (Subhaanahu wa Ta´ala) anapenda kusamehe. Anapenda kusamehe kuliko kuadhibu. Kwa ajili hii ndio maana anafurahi kwa tawbah ya mtu.

[1] al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/102)
  • Imechapishwa: 05/02/2023