Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

وعن أبي حمزة أنس بن مالك الأنصاري – خادم رسول الله صلي الله عليه وسلم – رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلي الله عليه وسلم: ((لله أفرح بتوبة عبده من أحدكم: سقط على بعيره، وقد أضله في أرض فلاة)) (متفق عليه)

15 – Hamzah Anas bin Maalik al-Answaariy (Radhiya Allaahu ´anh) – mtumishi wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah ni mwenye furaha mno kwa tawbah ya mja Wake kuliko mmoja wenu aliyeanguka kutoka juu ya ngamia wake na akampotea pindi alipokuwa katika ardhi ya jangwa.”[1]

Katika Hadiyth hii kuna dalili ya kufurahi kwa Allaah (´Azza wa Jall). Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anafurahi, anakasirika, anachukia na anapenda. Lakini hata hivyo sifa hizi sio kama sifa zetu sisi. Allaah amesema:

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye, Naye NdiyeMwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.” (42:11)

Ni furaha inayolingana na ukubwa na utukufu Wake. Sio furaha inayofanana na  furaha ya viumbe.

[1] al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/102-103)
  • Imechapishwa: 05/02/2023