Swali: Ni ipi hukumu ya kumfanyia uasi mtawala na ni zipi vigezo vyake?

Jibu: Hakuna yeyote mwenye mashaka kwamba ni haramu kumfanyia uasi mtawala muislamu. Allaah Ameharamisha kumfanyia uasi mtawala muislamu:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ

“Enyi mlioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi.” (04:59)

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ninakuusieni kumcha Allaah na kusikiliza na kutii hata kama mtatawaliwa na mtumwa. Hakika yule atayeishi katika nyinyi basi ataona tofauti nyingi. Hivyo basi, shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za makhaliyfah wangu waongofu baada yangu. Shikamaneni nazo bara bara na ziumeni kwa magego yenu. Tahadharini na mambo ya kuzua. Kwani hakika kila kitakachozushwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu na kila upotevu ni Motoni.”

Huu ndio mfumo salama ambao unatakiwa kufuatwa. Usiwajali wale ambao wanataka kuleta mfarakano kwa Waislamu na kutenganisha mkusanyiko na fitina. Huyu hatumjali. Bali tunatahadhari naye na kutahadharisha naye.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqo-01-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 03/05/2015