Swali: Je, magazeti ya “al-Bayaan” na “as-Sunnah” ni magazeti ya Salafiyyah?

Jibu: Kuhusu gazeti la “al-Bayaan” mwanzoni lilikuwa la Salafiyyah. Hata Muhammad Suruur mwanzoni alikuwa akiandika mambo mazuri. Wakati baada ya hapo akafungamana na Hizbiyyah na al-Ikhwaan al-Muslimuun ndipo akarudi katika chimbuko lake la mwanzo. Msingi wa malezi yake ni ya al-Ikhwaan al-Muslimuun. Muhammad Suruur ana malezi ya al-Ikhwaan al-Muslimuun ingawa alienda kinyume nao. Mwanzoni alikuwa akiandika mambo mazuri kwenye gazeti la “al-Bayaan”. Baada ya hapo akaanza kupinda. Kwa ajili hiyo linatakiwa kuitwa gazeti la “al-Bid´ah” na si gazeti la “as-Sunnah” na gazeti la“al-´Amaalah” (vibaraka) na si gazeti la “al-Bayaan”.

Baada ya hapo akaanza mashambulizi mengi, mengi na mengi kwa wanazuoni waheshimiwa wa Tawhiyd. Anasema kuwa ni waja wa waja wa waja ambaye bwana wao ni mnaswara. Kuna wanazuoni ambao ni watukufu – Allaah awajaze kheri – ambao hawatakiwi kuelezwa namna hiyo. Mtazamo wao juu ya fitina, maasi na mapinduzi ni mbora kuliko mtazamo wako wewe, ee Muhammad Suruur. Ni lini Allaah ameunufaisha Uislamu na waislamu kwa maasi na mapinduzi?

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy (d. 1422)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/sounds.php?sound_id=15
  • Imechapishwa: 14/08/2023