al-Qaradhwaawiy anataka Uislamu uendane na wakati wa sasa

Nataka kuzungumza kwa mnasaba wa maneno ya Shaykh Hamdiy ya kwamba baadhi ya vitabu vya Shaykh al-Qaradhwaawiy na kuwa anafuata mwenendo uleule kama wa al-Ghazaaliy.

Ni kana kwamba walisoma pamoja na wakachukua fikira moja.

Mwanafunzi: al-Qaradhwaawiy anamuona al-Ghazaaliy kama mwalimu wake.

al-Albaaniy: Ndivyo?

Mwanafunzi: Na ni mdogo kwake kiumri.

al-Albaaniy: Ni kweli, lakini hakuna tofauti kubwa kati yao.

Mwanafunzi: Ipo, Shaykh. Kati yao sio chini ya miaka isiyopungua kumi. Shaykh al-Ghazaaliy amefika miaka 78.

al-Albaaniy: al-Qaradhwaawiy ana miaka mingapi? Kuna kipindi fulani niliishi Qatar. Nilikuwa nikikutana na al-Qaradhwaawiy na al-Ghazaaliy. Sikuona tofauti hii kubwa. Lakini niliona kuwa walisoma pamoja.

Ninachokusudia ni kwamba wakaafikiana juu ya mfumo unaopinda kutokamana na Sunnah. Utamkuta al-Ghazaaliy akidhoofisha Hadiyth, basi al-Qaradhwaawiy anakuwa nyuma yake na mambo yanaweza kuwa kinyume chake. Wanakubaliana juu ya Hadiyth nyingi zilizo Swahiyh kwamba ni dhaifu. Miongoni mwa Hadiyth zilizotangaa zaidi ni zile zilizomo kwa al-Bukhaariy. Hadiyth hii kwa leo imekuwa ni njia ya kumtambua ni nani aliyepinda kutokana na Sunnah. Hadiyth hiyo inahusu maradhi ya leo. Ambaye anajua kuwa ugonjwa huo unapigwa vita na dini, basi husema:

”Hapana nguvu wala namna isipokuwa kwa msaada wa Allaah.”

Ambaye amepinda kutokamana na Sunnah, basi anajaribu kuamsha ugonjwa huo kwa kusema hapana neno kufanya hivo. Hadiyth hiyo nakusudia ile isemayo:

”Watakuwepo watu katika ummah wangu wanaohalalisha uzinzi, hariri, pombe na zana za muziki… ”

al-Ghazaaliy ameitupilia mbali. al-Qaradhwaawiy amefanya hali kadhalika na zaidi. Amemnukuu Ibn Hazm adh-Dhwaahiriy juu ya Hadiyth ya al-Bukhaariy ya kwamba ni Hadiyth iliyozuliwa. Haya hayasemwi na mtu anayejua kile kinachotoka mdomoni mwake. Kwa sababu Hadiyth iliyozuliwa ni ile iliopokelewa na mwongo na mzushi. Je, hayo yanapatikana ndani ya ”as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy? Kamwe. Pamoja na hivyo Hadiyth hii imepokelewa kwa njia nyingi zingine. al-Qaradhwaawiy anajua Hadiyth hiyo ipo kwa al-Bukhaariy na anajua namna wanazuoni wamepokea Hadiyth hiyo kwa njia zingine pindi walipomraddi Ibn Hazm. Hata hivyo akapuuzilia mbali ijtihada zote hizi za kielimu na akasema:

”Ibn Hazm anasema kuwa ni Hadiyth iliyotungwa.”

Hii ni dalili kwamba anataka kuendana na wakati wa kisasa. Anataka Uislamu uendane na matamanio ya kisasa. Mara nyingi hutumbukia katika hili na inaonekana kana kwamba nyuma kuna mambo yaliyojificha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (823)
  • Imechapishwa: 14/11/2022