4 – Kujitokeza kwa mnyama. Mnyama maana yake kilugha ni kila kinachotambaa juu ya ardhi. Makusudio hapa ni mnyama ambao atamtoa Allaah karibu na kusimama kwa Qiyaamah. Kujitokeza kwake kumethibiti kwa Qur-aan na Sunnah. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَإِذَا وَقَعَ الْقَوْلُ عَلَيْهِمْ أَخْرَجْنَا لَهُمْ دَابَّةً مِّنَ الْأَرْضِ تُكَلِّمُهُمْ أَنَّ النَّاسَ كَانُوا بِآيَاتِنَا لَا يُوقِنُونَ

“Na itakapowaangukia kauli [kwa uwazi wake] Tutawatolea mnyama atembeaye katika ardhi atakayewasemezesha [aseme] kwamba watu walikuwa hawana yakini na alama Zetu.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Qiyaamah hakitosimama mpaka muone kabla yake alama kumi” ambapo akataja miongoni mwazo mnyama.”[2]

Ameipokea Muslim.

Hamna ndani ya Qur-aan na Sunnah Swahiyh yanayofahamisha maeneo atapotokea mnyama huu na sifa zake. Hakika si venginevyo kumepokelewa juu ya hilo baadhi ya Hadiyth ambazo katika kusihi kwake zinahitajia kuangaliwa vizuri. Udhahiri wa Qur-aan ni mnyama unaowaonya watu juu ya kukurubia kwa adhabu na maangamivu. Allaah ndiye mjuzi zaidi.

[1] 27:82

[2] Muslim (2901, 39).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´aliyq mukhtaswar ´alaa Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 110
  • Imechapishwa: 13/11/2022