al-Qaradhwaawiy alikuwa na mambo mengi ya kikhurafi na kipotevu

Swali: Mmoja katika viongozi wa kizushi amekufa ambapo wakatofautiana ndugu kati ya kuonyesha fuuraha na wengine kutoonyesha. Ni nani aliye kwenye haki?

Jibu: Anapokufa muislamu, inatakiwa kutaja mazuri yake na kunyamazia mabaya yake. Ikiwa alikuwa na Bid´ah, basi tunazitahadharisha mbali na kumsema vibaya utu wake. Muislamu anatakiwa kuwatakia rehema maiti wa kiislamu wote. Hata hivyo hapana shaka kwamba bwana huyo aliyeashiriwa alikuwa na mambo mengi ya ukhurafi na fatwa za kipotevu. Tahadhari kutokana na fatwa zake. Kuhusu kumzungumzia na mafikio yake, jambo lake anaachiwa Allaah ndiye mwamuzi.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://darulhadith.com/al-qaradhawi-ar-dod/
  • Imechapishwa: 03/09/2023