07. Mama yake Mtume alikufa lini na ni nani aliyemtunza baada ya hapo?

Swali 7: Mama yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikufa lini? Alitunzwa na nani baada ya hapo?

Jibu: Mama yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifariki al-Abwaa´, baina ya Makkah na Madiynah, akiwa na miaka sita. Alikuwa njiani akirejea kutoka kwa wajomba zake Banuun-Najjaar. Baada ya hapo akaangaliwa na babu yake ´Abdul-Muttwalib.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 92-93
  • Imechapishwa: 03/09/2023