Magaidi na Khawaarij hawana lolote kuhusiana na Salafiyyah

Swali: Katika baadhi ya miji Salafiyyuun wanaelezwa kuwa ni magaidi, khaswa katika vyombo vya mawasiliano…

Jibu: Salafiyyah, Sunnah, Ahl-us-Sunnah, Uislamu, Ahl-ul-Hadith, kundi lililookoka na kundi lililonusuriwa ni majina ya kundi moja, ni wale wenye kushikamana na yale aliyokuwemo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake.

Kuhusu wale wenye kuhalalisha damu ya waislamu na wanajiita wao wenyewe majina yaliyopo hapo juu, ni jambo lisilofaa kwao. Hawastahiki majina haya. Ni kama mfano wa wale wanaojiita “masalafi wa kijihadi”. Wao si jengine isipokuwa ni waharibifu. Hawana lolote kuhusiana na jihaad, wala hawana Salafiyyah yenye uzito sawa na mdudumchungu. Kwa hivyo tujihadhari na hoja potofu.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://darulhadith.com/terrorister-och-khawaridj-har-ingenting-med-salafiyyah-att-gora/
  • Imechapishwa: 03/09/2023