al-Fawzaan kulipa swalah iliyomwingilia mwanamke wakati wa hedhi

Swali: Mwanamke akijiwa na hedhi baada ya kuingia swalah ya Dhuhr. Je, atapotwaharika aswali Dhuhr pamoja na Swalah ya ´Aswr?

Jibu: Hapana. Akiingiliwa na hedhi mwanzoni mwa wakati hana juu yake kitu kwa kuwa wakati ni mpana na hivyo atakuwa amepata hedhi kabla ya kuweza kuswali. Wakati wa swalah ni mpana. Hana juu yake kitu. Hili ni kinyume na yule mwenye kutwaharika mwishoni mwa wakati wa swalah. Huyu ndiye ambaye anawajibika kuswali swalah hiyo na iliyo kabla yake. Ama mwenye kupatwa na hedhi mwanzoni mwa wakati wa swalah hana juu yake kitu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (38) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-2-4_1.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020