Swali: Je, mama wa mke wa baba yangu na dada zake ni Mahram wangu?

Jibu: Hapana, sio Mahram zako. Mama wa mke wa baba yako ni Mahram kwa baba yako. Ama wewe huna mafungamano yoyote. Kadhalika hili ni kwa dada zake [wewe huna mafungamano yoyote nao]. Dada zake sio halali kwa baba yako. Vilevile dada za mke wake:

وَأَن تَجْمَعُوا بَيْنَ الْأُخْتَيْنِ

“Na [mmeharamishwa] kuwaoa dada wawili… ” (04:23)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (38) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-2-4_1.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020