Swali: Je, imeshurutishwa walii wa mwanamke atakayemuozesha awe amehifadhi swalah pamoja na mkusanyiko msikitini?
Jibu: Ndio. Ikiwa anaswali lakini haswali pamoja na mkusanyiko msikitni, huyu ni muasi na usimamizi wake haumtoki. Ama ikiwa haswali kabisa hata baadhi ya swalah, anaacha swalah kwa kukusudia, huyu ni kafiri na hapaswi kuwa walii wa Muislamu. Ni lazima awe na walii mwingine katika waislamu.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/12934
- Imechapishwa: 20/09/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Walii wa mwanamke haswali
Swali: Kuna mwanamke baba yake haswali. Je, yeye ndiye atakuwa walii atapotaka kuolewa? Jibu: Lipelekwe mahakamani. Kusema kwake haswali anakusudia kuwa haswali pamoja na mkusanyiko [msikitini] au haswali kabisa? Ikiwa haswali kabisa ni kafiri. Kafiri hawi walii wa muislamu mwanamke. Lakini alipeleke mahakamani.
In "Walii"
Mume anayepuuza swalah
Swali: Dada huyu anasema. Mume wake anapuuzia swalah na anamnasihi. Wakati mwingine anamuuliza: “Je, umeswali?”. Anasema: “Je, kwa nini? Kwani umeona mimi ni kafiri?” Anauliza, je, juu yangu nina dhambi? Je, niishi naye na tumeshakuwa na watoto? Kula na kunywa nyumbani kwake ni haramu? Jibu: Ikiwa ameacha swalah moja kwa moja…
In "Hukumu ya swalah ya mkusanyiko"
Mwenye kuswali swalah ya ijumaa tu ni afiri – asiyeswali katika jamaa´ah ni mnafiki
Swali: Kuna ambao hawaswali swalah za faradhi na hawahudhurii isipokuwa swalah ya ijumaa tu. Unasemaje juu ya hilo? Jibu: Ikiwa anaacha swalah za faradhi na haswali isipokuwa swalah ya ijumaa tu, huyu ni kafiri. Yule anayeswali swalah ya ijumaa pamoja na jamaa´ah na anaacha kuswali swalah zingine pamoja na jamaa´ah,…
In "Hukumu ya swalah ya mkusanyiko"