Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke kusoma Qur-aan na yuko na hedhi, ni mamoja kusoma kimoyoni au ndani ya msahafu, bila ya kuugusa?

Jibu: Wanachuoni wametofautiana katika hili. Madhehebu [ya Hanaabilah] yanaonelea kuwa haijuzu kwake kusoma. Kuna wanachuoni waliofutu, ikiwa ni pamoja vilevile na Shaykh Ibn Baaz, ya kwamba hakuna dalili ya wazi ya kumkatalia. Haya ndio maoni yake (Rahimahu Allaah). Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah anasema kuwa inajuzu kwake kusoma akichelea kusahau. Ikiwa ni mwanamke amehifadhi Qur-aan na anachelea kuisahau, inajuzu kwake kusoma ili kuiweka imara [hifdhi yake] ili asije akapitikiwa na kitu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (76) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-11-12.mp3
  • Imechapishwa: 22/08/2020